Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala Januari 23, 2024 amefanya Mkutano wa hadhara kwa nyakati tofauti katika Kata za Mahuta, Mdimba na Mnyawa akiwasisitiza Wananchi kufanya usafi katika makazi yao sambamba na kujenga Vyoo Bora ili kujilinda na Magonjwa yatokanayo na uchafu ikiwemo kipindupindu pamoja na Malaria.
Aidha, DC Sawala ameagiza kuwa ifikapo Februari 5, 2024 wananchi wote wawe na Vyoo katika maeneo wanayoishi .
Katika Mkutano huo DC Sawala amesikiliza kero mbalimbali za wananchi pamoja na kupatia majibu na ufumbuzi wa baadhi ya kero hizo na kuahidi kuendelea kushirikiana katika kuleta Maende
leo.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa