Na Kitengo cha Mawasiliano
Walengwa wa TASAF Halmshauri ya Wilaya ya Tandahimba wamepewa elimu ya lishe ili kuendelea kuimarisha afya
Elimu hiyo imetolewa na wawezeshaji kupitia Warsha za jamii katika Vijiji vyote ambapo wamesistiza umuhimu wa kuzingatia makundi matano ya vyakula ili kuwa na afya njema ili kuendelea kufanya shughuli zao za Maendele
Aidha naye Mratibu wa TASAF Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Ndg.Judicy Mnzava amewasistiza walengwa kuwa na matumizi sahihi ya fedha ikiwa sambamba na kuwekeza katika shughuli za kiuchumi,ununuzi wa mahitaji ya shule ya wanafunzi kwa kaya zenye wanafunzi ,kuwasimamia wanafunzi kuhudhuria shule na wale watoto chini ya miaka mitano wapelekwe kliniki
Malipo ya Walengwa wa TASAF Halmashauri yaWilaya ya Tandahimba yalianza Juni 14 hadi 19,2023 ambapo kiasi cha shilingi Milioni 430.5 zililipwa kwa kaya 7677 na kiasi cha Tsh.518,573 kwa kaya 13 hazikulipwa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo mlengwa kufariki,kutohudhuria wakati wa malipo na kuhama
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa