Na Kitengo cha Mawasiliano.
Viongozi ngazi ya Kata Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba wametakiwa kuhamasisha Jamii ujenzi wa vyoo bora na usafi wa mazingira katika maeneo yao ili kuepuka magonjwa yatokanayo na uchafu wa mazingira.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Ndg.Raphael Mputa kwenye kikao kazi kilichofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri amesema ni jukumu la viongozi kusimamia na kuhimiza usafi wa mazingira na ujenzi wa vyoo bora kwa Jamii.
" Viongozi mkazingatie maelekezo ya wataalamu waliyowapa,mkasimamie na mtoe elimu kwa wananchi katika mikutano yenu mnayofanya ili kuhamasisha ujenzi wa vyoo bora na usafi wa mazingira sambamba na kufanya kazi zenu kwa uadilifu" amesema Ndg.Mputa.
Kwa upande wa Wawezeshaji wamesistiza kuwa mkakati wa pamoja ni kusimamia na kuhimiza usafi wa mazingira na kila kaya iwe na vyoo bora na vibuyu chirizi kwa ajili ya kunawa mikono ili kuendelea kuimarisha afya bora kwenye jamii.
Aidha, wawezeshaji wameeleza kuwa takwimu sahihi zitachukuliwa kila robo ya Mwaka ambapo Wenyeviti wa Vitongoji watapita katika kila kaya kuona hali halisi na kuchukua taarifa za kaya husika ambapo kijiji kitakachofanya vizuri kitapewa fedha na Mradi wa WASH wa Lipa kwa matokeo (P4R)ambazo watazitumia katika shughuli zao za Maendeleo kwenye kijiji chao.
Kikao hicho kilianza Oktoba 12,2023 kimehitimishwa leo Oktoba 13,2023 ambapo kimehudhuriwa na Maafisa Tarafa,Watendaji Kata,Watendaji wa Vijiji, Wenyeviti wa Vijiji na Wenyeviti wa vitongoji
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa