Na Kitengo cha Mawasiliano.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Joshua Mgoli Septemba 15, 2023 ametembelea na kukagua Ujenzi wa Miundombinu ya Shamba Darasa la Ufugaji wa Viumbe Maji linalojengwa katika Kata ya Chaume .
Ujenzi wa Miundombinu hiyo utagharimu Tsh.Milioni 125.8 Fedha kutoka Serikali kuu ambapo tayari Mkandarasi ameanza kazi ya Ujenzi huo unaotarajiwa kukamilika ifikapo Mwezi Machi, 2024.
Aidha, Mradi huo unatarajia kuwanufaisha wananchi ambao watafundishwa kuandaa mashamba Yao ya Ufugaji wa Viumbe Maji wakiwemo Samaki ili kujiongezea kipato na kujikwamua kiuchumi.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa