Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) imekabidhi miradi yenye thamani ya shilingi milioni 100 kwa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba
Akikabidhi miradi hiyo ambayo ni madarasa matatu na matundu ya vyoo kwa baadhi ya shule za msingi Kaimu Mkurugenzi wa Tea John Masatu amesema kuwa miradi hiyo imekamilika na ipo tayari kuendelea kutumika na wanafunzi
Miradi wa madarsa matatu shule ya msingi Litemla
Akipokea miradi hiyo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji ,Afisa Elimu Msingi Hadija Mwinuka amesema kuwa wanaishukuru Tea kwa miradi hiyo ambayo imeleta tija kwa wanafunzi wa maeneo ambayo miradi hiyo imetekelezwa
Aidha amesema shule ambazo miradi hiyo imetekelezwa ni vyumba vitatu vya madarasa shule ya Msingi Litemla na matundu ya vyoo 24,shule ya Msingi Mitumbati matundu 24 ya vyoo,Shule ya Msingi Mnaida matundu 24 ya vyoo na Shule ya Msingi Namindondi matundu ya vyoo 24
Mradi wa matundu ya vyoo 24
“Tunashukuru kwa miradi hii ambayo imetekelezwa ndani ya Halmashauri yetu italeta mafanikio kwa wanafunzi wetu hususani katika maeneo ambayo matundu ya vyoo ilikuwa ni machache sasa imeleta nafuu,”amesema Mwinuka
vyumba hivyo vimekamilika na samani zake
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa