Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Zaidi ya shilingi Milioni 348 zimetumika katika zoezi la Uhaulishaji wa fedha kwa kaya maskini 5765 ambao walifanikiwa kuhakikiwa mwezi Julai Halamshauri ya Tandahimba
Mratibu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Ismaely Mbilinyi amesema kuwa zoezi limekamilika na kaya ambazo zimepata malipo hayo ni zile ambazo zilihakikiwa mwezi Julai mwaka huu
Mratibu wa TASAF Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Ismaely Mbilinyi akitoa maelekezo kwa wasimamizi wa malipo
“Tumemaliza zoezi la uhaulishaji wa fedha kwa kaya zote ambazo ziliingizwa kwenye mpango baada ya uhakiki mwezi Juni, na malipo ambayo yamefanyika ni mwezi Julai hadi Agosti na Septemba hadi Oktoba,zoezi limemalizika vizuri,”amesema Mbilinyi
Aidha amezitaka kaya ambazo zimepokea malipo hayo kuzitumia ipasavyo sambamba na kuwanunulia wanafunzi mahitaji muhimu ya shule,kilimo na ufugaji ili waweze kuendelea kukuza kipato
Msimamizi wa kituo cha Mahakamani kata ya Chikongola akiwa kufanya malipo
Naye Maimuna Lyoka mkazi wa Mchichira ameishukuru serikali na kuahidi kuzitumia kwa malengo pamoja na kufanya shughuli za ufugaji na kilimo ili kukuza kipato
Mpango wa Uhaulishaji wa Fedha kwa kaya maskini unaotolewa na TASAF umewezesha wanufaika wa Wilaya ya Tandahimba kuweza kuendelea kuwasomesha watoto wao kwa kuwanunulia mahitaji muhimu na wengine wakitoka hatua moja kwenda nyingine kwa kufanya shughuli mbalimbali za kukuza kipato
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa