Pichani: Baadhi ya viti vilivyotengenezwa na halmashauri vikiwa tayari kutumika
Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Zaidi ya Shilingi Milioni 2010 zimetumika kutengenezea viti na meza 3000 katika Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba baada yakuwa na changamoto ya upungufu wa viti na meza kwa shule za sekondari na hivyo kusababisha wanafunzi kusoma katika mazingira magumu
Akisoma taarifa fupi kwa Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba katika ghafla ya kukabidhi viti hivyo kwa baadhi ya walimu wakuu Afisa Elimu Sekondari Sostenes Luhende amesema viti hivyo vitagaiwa katika shule zote 28 za Halmashauri
“Fedha hii imetokana na mfuko wa elimu ambao unatiokana na mchango wa wananchi na wadau mbalimbali wa elimu,uwepo wa viti hivi umepunguza tatizop hili ambalo lilikuwa ni changamoto katika shule zetu za sekondari”amesema Luhende
Pichani Mkuu wa wilaya ya Tandahimba akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wilaya ya Tandahimba akikabidhi viti na meza kwa wakuu wa shule za sekondari
Mkuu wa Wilaya Sebastian Waryuba amewataka walimu wakuu kutunza viti hivyo kwa kutoa utaratibukwa wanafunzi waweze kuvitunza na pale utakapotokea uharibifu katika hilo aweze kuwajibika ili wengine waendelee kutumia
“Viti hivi ni agizo la mkuu wa Mkoa wa Mtwara ambaye aliiagiza Halmashauri kutengebneza viti na meza baada ya kutembelea shule na kuona hali halisi katika shule za sekondari,hivyo agizo limetekelezwa sasa ninyi walimu ambao leo tunawakabidhi viti hivi mkasimamie utunzwaji wa hivi viti”,amesema Waryuba
Wakuu wa shule wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa viti na meza
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa