Na Kitengo cha Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba na Mwenyekiti wa Kamati ya Sensa Wilaya Mhe.Kanali Patrick Sawala amesema Zoezi la Sensa ya Watu kwa kata zote 32 limekamilika
Amesema hay oleo Agosti 29,2022 katika kikao cha Kamati ya Sensa Wilaya ambacho kimefanyika katika ukumbi wa mikutano wa DC ambapo ameeleza kuwa leo makarani wanapita katika maeneo mbalimbali kuhakikisha endapo kuna mwananchi bado hajahesabiwa aweze kuhesabiwa
“Sisi Wilaya ya Tandahimba kata zetu zote 32 zimekamilisha Zoezi la Sensa ya Watu leo ni siku ya mwisho wa zoezi,gari la matangazo litaendelea kupita kuwakumbusha endapo kuna mwananchi hajahesabiwa kutumia siku ya leo kuhesabiwa,”amesema Dc Sawala
Zoezi la Sensa ya Watu leo Agosti 29,2022 linafikia mwisho ambapo wananchi wa Halmasahauri ya Wilaya ya Tandahimba wamehamasika na wametoaa ushirikiano kwa makarani katika maeneo mbalimbali ambayo walipita
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa