Na Kitengo cha Mawasiliano
Kuelekea Miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania Bara watumishi na Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba wameshiriki kufanya usafi wa mazingira na kupanda miti
Zoezi hilo limefanyika leo Disemba 7 ambapo wananchi wamefanya usafi katika maeneo yanayozunguka makazi yao,maeneo ya biashara na kando ya barabara ambapo zoezi hilo limekwenda sambamba na upandaji miti
Akizungumza mara baada ya zoezi la upandaji miti uliofanyika katika shule ya Msingi Mjimpya Katibu Tawala Wilaya ya Tandahimba Ndg.Juvenile Mwambi amesistiza miti hiyo kutunzwa ili iweze kuwa kumbukumbu nzuri ya miaka 61ya Uhuru
“Nawapongeza watumishi na wananchi wameshiriki katika maadhimisho haya ya upandaji miti na usafi wa mazingira tukiwa tunaelekea katika maadhimisho ya iaka 61 ya Uhuru,miti hii itakuwa kumbukumbu nzuri hivyo rai yangu miti hii itunzwe,”amesema Das
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa