Na Kitengo cha Mawasiliano.
Waziri Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Mhe.Dkt.Stergomena Tax amefanya ziara Wilaya ya Tandahimba na Kuzindua Mradi wa Maji Chitoholi katika Kata ya Mkundi.
Akizungumza na Wananchi mara baada ya Kuzindua Mradi huo Dkt.Tax amewataka Wananchi hao kutunza miundombinu iliyowekwa ili idumu kwa muda mrefu na waweze kunufaika.
"Nimetumwa na Mheshimiwa Rais wetu Dkt.Samia Suluhu Hassan kuwaambia anawapenda sana na anawapenda kwa vitendo kama mnavyoona mradi huu ni Mkubwa, na Kufikia Mwezi Juni 2025 maji yatawafikia Wananchi kwa 90%" Dkt.Tax
Awali akisoma taarifa ya Mradi huo Meneja wa RUWASA Wilaya ya Tandahimba Mhandisi Antidius Muchunguzi amesema mradi huo umegharimu kiasi cha Tsh Bilioni 1.4 ikiwa ni fedha kutoka Serikali kuu kupitia mradi wa P-for-R ambapo zaidi ya Wananchi 10,817 sawa na 4% ya wakazi wa Tandahimba wananufaika na mradi huo .
Aidha, Mbunge wa Jimbo la Tandahimba ameishukuru Serikali kwa mradi huo akiwasisitiza Wananchi kuendelea kuiamini Serikali ya Samia Suluhu Hassan kwa kuwa inatekeleza kwa vitendo na kutatua kero za Wananchi ikiwemo kumtua mama ndoo.
Baadhi ya Wananchi wametoa maoni yao juu ya mradi wakisema wanaridhishwa na Kasi ya Maendeleo yanayofanyika katika Wilaya hiyo ikiwemo Miradi ya Maji.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa