Shirika lisilo la Kiserikali la RIDHAA FOR DEVELOPMENT FOUNDATION (RIDEFO) limetoa mafunzo kwa Wananchi wa Kata ya Mkonjoano Wilayani Tandahimba na kutoka Elimu ya kujenga na kuilinda amani huku likitoa mbinu za kutatua Migogoro miongoni mwa jamii .
Awali akifungua mafunzo hayo Mkurugenzi wa Shirika hilo Zuwena Musa amesema Maendeleo ya Jamii na nchi kwa ujumla hujengwa palipo na amani .
"Mimi na wewe tunahitaji amani hivyo tutajifunza mengi kuhusu namna ya kutunza amani ambayo ni Moja ya Tunu ya Taifa letu" Bi.Zuwena
Baadhi ya mafunzo yaliyotolewa na Mwezeshaji Festo Sing'ombe ni pamoja na kutatua migogoro isiyo ya lazima kwa njia ya mazungumzo, kuepuka matumizi ya lugha zisizofaa, kutenda kwa haki na usawa miongoni mwa jamii ili kujenga Jamii yenye amani na Mshikamano.
Aidha, Wananchi wamelishukuru Shirika hilo kwa kuwajengea uwezo na kuahidi kuwa mabalozi wa amani kwa jamii inayowazunguka.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa