Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe.Kanali Patrick Sawala akiambatana na Katibu Tawala Mkoa pamoja na Viongozi wengine wa Mkoa huo amekagua maendeleo ya miradi inayotarajiwa kupitiwa na Mwenge wa Uhuru Wilaya ya Tandahimba na kupongeza utekelezaji wake akisisitiza kufanyia kazi maboresho madogo madogo ili iendelee kuwa bora zaidi na kufaa kupitiwa na Mwenge.
Kwa Upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara Bahati Geuzye amesema Miradi inaridhisha na Kusisitiza nyaraka ziwepo eneo pa mradi kwa ufafanuzi.
Aidha, Mwenge wa Uhuru ifikapo Juni 2, 2024 unatarajia kupitia Miradi mbalimbali ya Wilaya ya Tandahimba ikiwemo Sekta ya Maji, Afya, Elimu, Miundombinu ya Barabara, Shamba la Miti sambamba na Uwezeshaji wa Vijana kiuchumi kupitia Mapato ya ndani .
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa