Na Kitengo cha Mawasiliano.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe.Kanali Patrick Sawala amefanya ziara Wilaya ya Tandahimba na kuzungumza na AMCOS, watunza maghala na wasafirishaji kuhusu kujiandaa vyema kutoa huduma na kutimiza wajibu wao katika Msimu wa Korosho unaotarajiwa kuanza Mwishoni mwa Mwezi Oktoba.
Kanali Sawala ametoa Rai kwa Viongozi hao akiwataka kuhakikisha wanasimamia ipasavyo Wakulima ili waweze kuuza Korosho Bora na kujikwamua kiuchumi.
"Tandahimba tuanze Msimu Vizuri, wahudumieni Wananchi vizuri kwa kufuata Sheria, kanuni, taratibu na miongozo iliyowekwa hakikisheni mnazingatia Ubora wa Korosho ghalani ili tuendelee kuwa na Sifa ile ile ya kuzalisha Korosho Bora"amesisitiza
Katika Ziara hiyo RC Sawala ametembelea Mradi wa Maji Chitoholi sambamba na Kituo Cha Afya Mihambwe kuona huduma za maji na Afya zinavyotolewa kwa Wananchi.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa