Na Kitengo cha Mawasiliano
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe.Kanali Ahmed Abbas Ahmed amesistiza umoja na mshikamano katika kutekeleza majukumu mbalimbali ngazi ya Mkoa ili kuunganisha nguvu kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu
Amesema hayo Aprili 26, 2023 katika kilele cha maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambapo Kimkoa yamefanyika katika kijiji cha mchichira Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba ambayo kauli mbiu inasema "Umoja na Mshikamano ndiyo nguzo ya kukuza Uchumi wetu "
Aidha Mkuu wa Mkoa amekabidhi zawadi kwa washindi mbalimbali walioshinda katika mashindano ya insha,timu za mpira,watoa burudani na skauti katika maadhimisho hayo
Naye Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Ndg.Mussa Gama akisoma taarifa yake ameipongeza Serikali kwa kuendelea kutoa fedha za miradi ya Maendelea ambapo imeboresha huduma ya afya,maji,elimu na Barabara katika Halmashauri ya Tandahimba
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa