Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Brig.Jen. Marco Gaguti amesema ameridhika na ubora wa kazi inayofanyika ya maendeleo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba
Ameyasema hayo jana Desema 10,2021kwenye ziara ya kukagua maendeleo ya vyumba vya madarasa Wilayani Tandahimba na kushauri kuwa katika miradi mingine yote inayoendelea kujifunza kupitia miradi hii ya Uviko -19
“Kwenye ziara hii ambayo nimefanya katika Mkoa wa Mtwara nimeridhika na maendeleo ya miradi inayoendelea katika Wilaya zote ikiwemo hii Tandahimba,lakini lipo jambo la kujifunza katika miradi hii tujitathimini na tujipange kuikamilisha miradi yote ambayo fedha yake ipo iweze kukamilika kwa wakati kabla ya mwaka wa fedha haujakwisha,”amesema Rc Gaguti
Aidha amesema sambamba na miradi hiyo ya elimu kuna mdondoko wa wananfunzi na ufaulu ambavyo vimekuwa ni changamoto na kuwataka wazazi,walezi na madiwani kuhakikisha wanasimamia suala la elimu katika maeneo yao na kuhakikisha wananfunzi wanapata chakula shuleni
Naye Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Kanali Patrick Sawala amesema kuwa miradi hiyo imetekelezwa kwa ushirikiano mkubwa wa viongozi ngazi ya Halmshaauri,madiwani,viongozi wa chama cha Mapinduzi na kamati,wakuu wa shule,watendaji na wananchi kila mmoja kwa nafasi yake ameweza kushiriki katika miradi hii
“Miradi yetu ipo katika hatua ya ukamilishaji hadi kufikia tarehe Desemba 13 tunatarajia kukukabidhi miradi hii ya vyumba vya madarasa 88 na ofisi 41 za walimu,”amesema Dc Sawala
Aidha naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Ndugu Mussa Gama amesema baada ya kupokea fedha kutoka Serikali kuu za ujenzi wa vyumba vya madarasa 88 ambayo gharama yake ni shilingi Bilioni 1.76 Halmashauri imeweza kujiongeza kujenga ofisi 41 katika kila mradi
“Baada ya kupokea fedha hizi tulijiongeza kwa kila mradi wa vyumba vya madarasa tumejenga na ofisi za Walimu ili waweze kukaa katika mazingira bora,”amesema Mkurugenzi
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa