Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa amewataka wakulima Wilayani Tandahimba kuondoa mikorosho iliyozeeka na kupanda mikorosho mipya ili kuongeza uzalishaji wa zao hilo
Ameyasema hayo kwenye ziara yake ya kampeni ya ondoa mapori ongeza uzalishaji Wilayani Tandahimba ambapo ametembelea mashamba kata ya Chingungwe, Luagala na Mkoreha na kusitiza kuendelea kulima mazao mengine yanayokubali katika maeneo husika
Rc Byakanwa akionyesha Mikorosho iliyozeeka ambayo haiwezi kuzalisha ipasavyo
“ Tandahimba ni Wilaya inayoongoza kwa uzalishaji hapa nchini na wanunuzi wa Kimataifa wanajua hivyo lakini uzalishaji unapungua kwakuwa mikorosho iliyopo mingi imezeeka ,na hakuna mapori mengi yaliyotelekezwa ila tatizo la hapa ni mikorosho ya siku nyingi haina nguvu ya kuzalisha ipasavyo kwahiyo tuiondoe tupande mbegu bora”amesema Rc Byakanwa
Rc Byakanwa akisistiza wananchi kubadilika ili kuongeza uzalishaji wa zao la korosho
Aidha akitoa takwimu ya uzalishaji Wilaya ya Tandahimba kwa wananchi amesema mwaka 215/2016 ilizalisha tani 40,000,mwaka 2016/2017 tani 70,000,mwaka2017/2018 tani 74,000,mwaka 2018/2019 tani 37,000,mwaka 2019/2020 tani 37,000 na msimu unaoendelea tani 25000 hadi sasa zimeuzwa
Dc Sebastian Waryuba akitoa neno kwa wananchi wa kijiji cha Kuchele kata ya Chingungwe
Naye Mbunge wa Jimbo la Tandahimba Mheshimiwa Katani Ahmad Katani (CCM) amesema anaunga mkono kampeni hiyo na atahakikisha wananchi wa Jimbo hilo hususani wakulima wanafuata kanuni za kitaalamu kwa kuondoa mikorosho iliyozeeka na kupanda mipya kwakuwa zao hilo ni uchumi wa wananchi wa Tandahimba
Mheshimiwa Katani(Mb) akimpongeza RC kwa kuanzisha kampeni hiyo ili kukuza uzalishaji wa zao la korosho
“Nakushukuru Rc kwa kuja na kampeni hii mimi nitashirikiana na viongozi wa Wilaya kusimamia hili kwa wakulima wetu kuweza kuondoa mikorosho ambayo imezeeka na kupanda mikorosho ya kisasa ili kuongeza uzalishaji,”amesema Mheshimiwa Katani
Pichani kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji (W)Said Msomoka ,wakuu wa Idara na Maafisa Tarafa ambao waliambatana na Rc katika ziara hiyo
Hata hivyo baada ya ziara hiyo wananchi katika maeneo hayo wameonyesha kuhamasika na kampeni hiyo na wataalamu kutoka Kituo cha Utafiti cha Naliendele na Bodi ya korosho Tanzania wameahidi kutoa ushirikiano kwa wakulima ili kuongeza uzalishaji
Wananchi wakishuhudia jinsi ya ukataji sahihi wa mikorosho ili iweze kubebeshwa mbegu mpya kutoka kwa mtaalam kutoka kituo cha utafiti Naliendele
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa