Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Afisa Sayansi ya Jamii Mkuu Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) Gibson Mwaya amesema ujenzi wa barabara ambayo aliahidi Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli kwa wananchi wa Tandahimba unatarajia kuanza mwishoni mwa mwaka huu 2020
Akizungumza na wakuu wa idara na vitengo katika ukumbi wa Halmashauri ya Tandahimba amesema kuwa pamoja na ujenzi huo kutarajia kuanza watalipa fidia kwa vitu ambavyo vipo mita 45 kutoka katika barabara ambayo wanatarajia kuanza kuitengeneza
Afisa Sayansi ya Jamii Mkuu wa Tanroads Gibson Mwaya akieleza lini mradi huo utaanza
“Dhumuni la kuongea nanyi wataalaum wa Halmashauri ni kupata ushauri na maoni yenu ambayo yatasaidia katika ujenzi huu mkubwa wa barabara ambayo Mheshimiwa aliahidi kwa wananchi na utekelezaji wake unaanza mara tu taratibu mbalimbali zikimalizika hivyo mwishoni mwa mwaka huu tutaanza rasmi kazi ya ujenzi wa barabara,”amesema Mwaya
Amesema barabara hiyo ikikamilika itawasaidia wakazi wa Tandahimba na Watanzania kwa ujumla kuweza kutoka sehemu moja kwenda nyingine kwa wakati na kwa gharama nafuu hivyo barabara hii itaongeza maendeleo kwa wakazi wake
“Sisi kama Tanroads kabla ya kuanza ujenzi tunashirikisha wananchi na wataalamu mbalimbali wa Halmashauri ili kupata maoni na ushauri hivyo pamoja na maendeleo tunayoleta pia tunaipa Halmashauri husika kuchagua kitu ambacho kingependa kifanywe ndani ya mradi huo ambao sisi tunaita ‘Complimentary Project’inategemea wanahitaji nini mfano kuchimbiwa kisima au kujengewa ghala na fedha ambayo imetengwa,”amesema Mwaya
Wakuu wa Idara na vitengo wakimsikiliza Afisa kutoka Tanroads kuhusu ujenzi wa barabara
Naye Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba amemshukuru Mheshimiwa Rais John Magufuli kwa kutekeleza ahadi yake kwa wananchi wa Wilaya ya Tanadahimba ambao suala la barabara limekua tatizo la muda mrefu
Dc Waryuba (kushoto) akitoa salamu za shukrani kwa Rais Magufuli (kulia) Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Tandahimba Said Msomoka
Barabara inayotarajiwa kujengwa ni kutoka Mnivata hadi Masasi ikikamilika itakuwa imewasaidia wananchi wa maeneo husika na kuwaletea maendeleo mbalimbali .
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa