Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Benki ya NMB tawi la Tandahimba imekabidhi madawati 150 kwa shule tatu za msingi na mabati 170 kwa ajili ya Zahanati ya Mitumbati vifaa vyote vikiwa na gharama ya shilingi Milioni 20
Katibu Tawala Wilaya ya Tandahimba Juvenile Jaka Mwambi akizungumza jambo
Akipokea vifaa hivyo Katibu Tawala Wilaya ya Tandahimba Juvenile Jaka Mwambi kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya amesema kuwa benki hiyo inawajali wananchi wake kwa kurudisha faida wanayoipata kwa jamii
Meneja wa benki ya Nmb tawi la Tandahimba akizungumza na wananchi wa kijiji cha mitumbati kabla ya makabidhiano ya mabati
“Tunaishukuru NMB kwa madawati na mabati ni matumaini yangu haya madawati yatatunzwa ili wananfunzi waendelee kuyatumia na kuongeza ufaulu kwa watoto wetu,”
Das(wa pili kulia) akiwa na Kaimu Mkurugenzi,Afisa Elimu na Meneja wa Kanda ya kusini na Meneja wa Tawi la Tandahimba kwenye ghafla hiyo
Naye Meneja wa Benki ya NMB kanda ya Kusini Janeth Shango amesema kuwa ni utaratibu wa benki hiyo kushiriki katika maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu na afya
Meneja wa Nmb Kanda ya Kusini Janeth Shango akiwasalimia wananfunzi na wazazi waliohudhuria katika makabidhiano hayo
“Tupo karibu na wananchi hata yakitokea majanga sisi tunakuwa karibu kushirikiana na Halmashauri yetu,kwaiyo ni utaratibu wetu kurudisha faida tunayipata kwa wananchi we,”amesema Shango
Hata hivyo naye Afisa Elimu Msingi amesema kuwa anaishukuru Benki hiyo kwa msaada wa madawati kwakuwa yataongeza ufanisi wa kusoma kwa wanafunzi katika shule zetu
“Hii ni benki ambayo tunashirikiana nayo sana katika sekta ya elimu,kwa msaada huu wa madawati hata mahudhurio yataongezeka,watoto watakuwa mwandiko mzuri kwakuwa mwanafunzi akikaa chini hata mwandiko wake unakuwa mbaya,”amesema Mwinuka
Zahanati ya Mitumbati ambayo benki ya Nmb imekabidhi bati 170 kwa ajili ya kuongeza nguvu
Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Hassan Nzyungu amewashukuru NMB na kuwaomba kuendelea kushirikiana na Halmashauri katika sekta mbalimbali ili kuleta maendeleo kwa wananchi wa Tandahimba
Das Juvenile Jaka Mwambi akimkabidhi mabati 170 Kaimu Mkurugenzi Hassan Nzyungu ambayo yametolewa na Nmb
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa