Na Kitengo cha Mawasiliano.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe.David Silinde amezindua mfumo wa upimaji wa mazao ya wakulima kupitia mizani ya kidigitali iliyounganishwa na mfumo wa usimamizi wa vyama vya ushirika ( MUVU).
Uzinduzi huo umefanyika leo Disemba 5,2023 kwenye eneo la maghala ya Chama Kikuu cha Ushirika Tanecu ambapo Mhe. Silinde ameagiza vyama vyote vya ushirika kutumia mizani ya kidigitali sambamba na kuhakikisha mtandao huo unapatikana vijijini kwa uhakika kwenye amcoss ili wakulima wapate huduma kwa ufanisi.
"Nimezindua rasmi mfumo huu na zoezi la usambazaji wa mizani ya kidigitali ambapo itakwenda kupunguza malalamiko ya wakulima ya kupunjwa kwa kilo za mazao yao wanapopeleka sokoni na mfumo huu utaongeza ufanisi na utendaji kwenye vyama vya ushirika," amesema Mhe.Silinde.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe.Kanali Patrick Sawala amesema mfumo huu utamsaidia mkulima kila atakapopima kupata ujumbe kwenye simu yake ambao utasaidia kupunguza malalamiko na ametoa wito kwa wataalamu kutoa elimu zaidi
Aidha kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Tandahimba Mhe.Katani Katani ameiomba Serikali kuchukua hatua za Kisheria kwa wanunuzi wanaotaka kuhujumu Korosho ya Tanzania.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa