Na Kitengo cha Mawasiliano
Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndg.Mary Chatanda ameridhishwa na mradi wa ujenzi wa Shule mpya ya Msingi na Awali Mambamba ambayo imetekelezwa kwa kiasi cha Tsh.Mil 331.6 kupitia mradi wa BOOST
Akizungumza Julai 20,2023 katika ziara yake ya siku moja katika Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba aliyoambatana na Kamati ya Utekelezaji ya UWT Taifa ambayo imetembelea na kukagua utekelezaji wa miradi ya Maendeleo sambamba na kuzungumza na wananchi
" Nimefurahi kuona jinsi utekelezaji wa ilani ya CCM inavyotekelezwa kwa vitendo katika miradi ya maendeleo hapa Tandahimba ,nawapongeza sana kwa usimamizi mzuri,mradi ni mzuri kwakweli nimeanza vizuri ziara yangu ," amesema Mwenyekiti Chatanda
Chatanda amesema kuwa miundombinu inayojengwa katika maeneo mbalimbali hapa nchini kama watoto hawatahudhuria shule haitakuwa na maana hivyo ni jukumu la wazazi na walezi kuhakikisha watoto wa kike na kiume wanakwenda shule kupata elimu ambayo itawasaidia kufikia malengo yao
Aidha ametoa wito kwa jamii kuzingatia mila na desturi za kulinda maadili ya Kitanzania ambayo yameanza kuleta madhara kwa baadhi ya vijana wa Kitanzanis sambamba na kupinga vitendo vya ukatili na unyanyasaji kwa wanawake na watoto
Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba ilipokea fedha kiasi cha Tsh.Mil.665.1 ambayo imetekeleza ujenzi wa miundombinu katika Shule za msingi saba ikiwemo mradi wa Shule mpya Mambamba kupitia Mradi wa BOOST ambayo tayari miradi hiyo imekamilika
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa