Na Kitengo cha Mawasiliano
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Mhe.Baisa Baisa ametoa Shukrani kwa Mhe.Rais kwa kutupatia fedha kiasi cha Shilingi Milioni mia mbili (Tsh.200,000,000) kwa ajili ya utekelezaji wa ujenzi wa vyumba vya madarasa kumi ikiwa ni maandalizi ya wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2023
Amesema hayo Oktoba 12,2022 kwenye kikao cha Wasimamizi wa miradi katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri
“Tunamshukuru Mhe.Rais kwa fedha hizi za ujenzi wa vyumba vya madarasa,Mhe Rais ameendelea kutukumbuka wanaTandahimba nasisi madiwani wa Tandahimba tupo naye bega kwa bega kusimamia miradi hii ikamilike kwa wakati na ubora,’amesema Mwenyekiti
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa