Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba imekabidhi viti na meza za wanafunzi wa shule za sekondari kwa ajili ya kidato cha kwanza mwaka 2021 kwa Wakuu wa Shule za sekondari hatua ambayo imemaliza tatizo la ukosefu wa viti na meza kwa wanafunzi
Meza na viti vikishushwa kwenye gari kwa ajili ya makabidhiano
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Tandahimba ndugu Ally Machela amesema kuwa jukumu ambalo wakuu wa shule wanapaswa kulizingatia ni kuhakikisha wanaweka utaratibu kwa wanafunzi ambao wanatumia viti hivyo ili viweze kudumu
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Ally Machela akitoa neno kwa wakuu wa shule kwenye makabidhiano ya viti na meza
“Tumetumia kiasi kikubwa cha fedha za mapato ya ndani kwa ajili ya kutengeneza samani hizi jukumu kubwa mnalo wakuu wa shule ni kuweka utaratibu ambao mwananfunzi atatunza kiti na meza atakazokabidhiwa,”amesema ndg Machela
Wakuu wa shule za sekondari wakisikiliza taarifa fupi ya ugawaji wa viti na meza hizo
Akikabidhi samani hizo Mwewnyekiti wa Halamsahauri ya Wilaya ya Tandahimba Mheshimiwa Baisa Baisa amaesema kuwa Halmashauri imetimiza jukumu la kutengeneza samani ili wanafunzi wasome katika mazingira bora hivyo uwekwe utaratibu ili samani hizi zisiwe zinarudiwa kila mwaka kutengenezwa
Mwenyekiti Mh.Baisa Baisa akimkabidhi viti Mkuu wa shule ya sekondari Nandonde bi. Mboni Ahmad
“Nakabidhi samani hizi lakini wekeni utaratibu wa mwanafunzi kutunza samani zake,azitunze kuanzia anaanza kidato cha kwanza hadi anapomaliza na endapo vitaharibika mzazi wake achukue hatua ya kutengeneza hii itasaidia kuwajenga wanafunzi wetu kuthamini na kutunza mali za umma,”amesema Mh. Baisa
Naye Mwenyekiti wa Walimu Wakuu wa Shule za Sekondari Tandahimba Ally Matangaru ameishukuru Halmashauri kwa jitihada wanazozifanya kwenye sekta ya Elimu na hivyo kuahidi kuendelea kuweka juhudi kwenye kutoa elimu ili kuongeza ufaulu katika Halmashauri ya Tandahimba
Mh.Mwenyekiti akimkabidhi meza Mwenyekiti wa Wakuu wa Shule ambaye pia ni mkuu wa shule ya sekondari Namikupa
Aidha akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Katibu Tawala Juvenile Mwambi ameipongeza Halmashauri kwa jinsi ambavyo imefanikisha zoezi la ukamilishaji wa samani hizo
Katibu Tawala akitoa neno la pongezi kwa Halmasahauri kwa kukamilisha zoezi hilo
Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba imetoa kiasi cha zaidi ya Milioni 145 katika Mfuko wa Elimu kwa ajili utengenezaji wa viti 2552 na meza 2492 ili kuondoa changamoto ya upungufu wa samani hizo kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza 2021
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa