Na Kitengo cha Mawasiliano
Halmasahauri ya Wilaya ya Tandahimba inatarajia kupokea Mwenge wa Uhuru Aprili 5,2023 ambapo utatembelea miradi ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni nne
Akiwasilisha taarifa katika kikao cha pili cha wadau wa maandalizi ya Mwenge wa Uhuru Februari 17,2023 kilichofayika katika ukumbi wa mikutano wa Halmasahauri Mratibu wa Mwenge wa Uhuru Wilaya ya Tandahimba Ndg Deodatus Mchwampaka ameeleza kuwa Mwenge wa Uhuru ukiwa Tandahimba utakimbizwa km 57.5 kuanzia eneo la mapokezi Miuta hadi eneo la makabidhiano Newala Mji
Naye mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba ambaye ni Katibu Tawala Ndg.Juvenile Mwambi amewasistiza wadau wa maandalizi ya Mwenge wa Uhuru kuendelea kushirikiana kila hatua ili kuweza kufanikisha mapokezi hayo sambamba na ushiriki wao kuanzia mapokezi hadi makabidhiano
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa