Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba imetoa unga kilo 1000 na maharage kilo 500 kwa familia zilizopata maafa ya mvua iliyoambatana na upepo mkali na kusababisha mtu mmoja kufariki dunia kwa kupigwa na radi na zaidi ya familia 48 zimekosa makazi
Tukio hilo limetokea kata ya Kwanyama Wilayani Tandahimba ambapo mvua hiyo iliyoambatana na upepo kunyesha na kusababisha maafa kwa wananchi wa kijiji cha Mitumbati ,kwanyama na huruma ambapo mikorosho imekatika ,vyakula vimeloa na mvua na nyumba kuezuliwa na zingine kubomoka
Dc Sawala akiwa pamoja na viongozi wa Wilaya wakiangalia jinsi mvua hiyo ilivyoleta maafa
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala alitembelea kuona na kutoa pole kwa waathirika wa maafa hayo katika kata hiyo na kuwasistiza kuhakikisha wanafunga koha paa ziwe imara ili endapo upepo unarudi usiweze kuleta maafa tena
Aidha Dc Sawala akikabidhi vifaa hivyo amesema kuwa ulinzi utaimarishwa ili kuendelea kulinda mali za wananchi ambao wamekosa makazi hadi pale hali itakapokuwa sawa
Afisa Tarafa Mchichira bi Dotto Nyirenda akishirikiana na wananchi kuhifadhi chakula hicho kwa ajili ya kugawa kwa wananchi
“Nachukua nafasi hii kutoa pole kwa wafiwa lakini pia natoa pole kwa wale wote ambao wamepata maafa haya lakini kitu muhimu tukiwa tunaanza kuezeka basi tuhakikishe koha zinafungwawa ili kuepuka mili kuepukaka maafa
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Mhe.Baisa Baisa ametoa pole kwa wananchi wa kata ya Kawanayama na kuwakikishia kuwa Halmashauri ipo pamoja nao kuhakikisha wanapata chakula na michakato mingine inaendelea
Diwani wa Kata ya Kwanyama Mhe Hamza Balakali ameishukuru Serikali ya Wilaya kwa kufika na kuwafariji wananchi waliopata maafa hayo sambamba na kuwapa msaada wa chakula
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa