Na Kitengo cha Mawasiliano
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara Nanjiva Nzunda amesema baada ya Mafunzo ya Mfumo wa Ununuzi kwa njia Mtandao (NeST) kukamilika , anatarajia kuona Mkoa wa Mtwara unakuwa wa Mfano katika matumizi ya Mfumo huo
Nanjiva ameyasema hayo wakati wa kufunga mafunzo ya Mfumo huo kwa wataalamu wa Halmashauri Sita za Mkoa wa Mtwara
Aidha Nanjiva amewasisitiza wataalamu kutumia Mfumo huo ili kuondokana na Faini itakayotozwa kwa Halmashauri itakayofanya manunuzi nje ya Mfumo wa NeST.
"Nategemea kwamba Faini ya Tsh. Milioni 10 tutaiepuka kwa kuwa tayari tutakuwa tunatumia Mfumo kuanzia Oktoba 1, 2023,"amesema Nanjiva.
Kwa Upande wao wataalamu waliohudhuria mafunzo hayo ya Siku Tano wamesema wako tayari kutumia Mfumo huo wa Ununuzi kwa kuwa ni rahisi pia.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa