Na Kitengo cha Mawasiliano
Msimamizi wa Uchaguzi ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Ndg.Mariam Mwanzalima amemtangaza diwani wa Kata ya Luagala Mhe.Rehema Liute(CCM) kuwa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba kwa kupata kura 37 kati ya kura 39 za wajumbe walioshiriki uchaguzi huo
Akisoma matokeo hayo leo Agosti 24,2023 katika Mkutano wa kawaida wa mwaka wa fedha 2022/2023 uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano amesema kuwa wagombea wawili wa nafasi hiyo Mhe.Sharafi Ngajime diwani wa Kata ya Mdimba kutoka Chama cha ACT-WAZALENDO ambaye amepata kura 2 na Mhe.Rehema Liute diwani Kata ya Luagala kutoka Chama cha Mapinduzi ambaye amepata kura 37
Aidha Ndg.Mwanzalima amesema kuwa jumla ya kura zote za wajumbe zilikuwa 39 na hakuna kura iliyoharibika
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa