Na Kitengo cha Mawasiliano.
Chama Kikuu cha Ushirika Tandahimba na Newala(TANECU) kimefanya Mnada wa kwanza wa zao la Korosho kwa Msimu wa kilimo Cha Korosho 2023/2024 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba ambapo Korosho imeuzwa kwa Bei ya juu ya Tsh.2050 na Bei ya Chini Tsh.1950 Kwa kilo moja.
Mwenyekiti wa TANECU Karim Chipola amewasisitiza Wakulima kuziandaa Korosho kwa Ubora kabla ya kuzipeleka ghalani.
"Ukipeleka Korosho Mbichi ghalani inaharibu soko na kushusha Bei, niwasisitize endeleeni kuzikausha na kuepuka kuongeza vitu ambavyo siyo Korosho " Chipola
Akisoma hali ya Ukusanyaji wa Korosho kwa Mnada wa kwanza Meneja wa TANECU Mohamed Nassoro amesema Jumla ya Tani 7752 zimekusanywa ambapo kati ya hizo Tandahimba imekusanya Jumla ya Tani 5981.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba,Kaimu Katibu Tawala Wilaya hiyo Francis Mkuti ameishukuru Serikali kwa kutoa Pembejeo kwa wakulima Bure hali iliyopelekea Uzalishaji wa Korosho kuongezeka
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa