Na Kitengo cha Mawasiliano
Katika Kusherekea miaka 61 ya uhuru wananchi na watumishi kila mmoja kwa nafasi yake wametakiwa kufanya kazi kwa bidii ili kuleta mabadiliko chanya katika Wilaya na Taifa kwa Ujumla
Akizungumza katika Kongamano la Maadhimisho ya Miaka 61 ya Uhuru ambalo limefanyika katika Ukumbi wa Mikutano leo Disemba 9,2022 Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala amesistiza kuwa usipofanya kazi na kutimiza wajibu wako hauwezi kuwa Huru
“Kila mmoja afanye kazi kwa bidii katika nafasi yake na kuhakikisha vitu chanya vinatokea,heshima yako na uhuru wako ni pamoja na kufanya kazi ,tunaposherekea Uhuru wa miaka 61 tujitathimini ,wewe kama mtanzania unailetea Tanzania maendeleo, jitathimini kwanza wewe binafsi,”amesema Dc Sawala
Aidha nao wadau mbalimbali waliochangia katika mdahalo huo wameipongeza Serikali kwa mabadiliko yaliyopatikana kwa kipindi cha miaka 61 ambapo katika Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba mabadiliko yanaonekana katika sekta mbalimbali
Katika Maadhimisho ya miaka 61 ya Uhuru Dc Sawala aliwakabidhi washindi wa Insha zawadi mbalimbali sambamba na washindi wa michezo katika maadhimisho hayo
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa