Na Kitengo cha Mawasiliano
Mbunge wa Jimbo la Tandahimba Mhe.Katani Katani amemshukuru Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kutoa fedha za miradi ya Maendeleo kwa wananchi wa Tandahimba
Amesema hayo Julai 20,2023 katika ziara ya Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndg.Mary Chatanda katika Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba baada ya kumpa nafasi ya kuzungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara ambapo alieleza kuwa fedha hizo zimetekeleza miradi ya maji,umeme,barabara,vyumba vya madarasa na vituo vya afya
" Sisi wanaTandahimba tunamshukuru Mhe.Rais kwa Mabilioni ya fedha ya kutekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo kwa kipindi hiki cha miaka miwili na miezi mitatu ya kuwa madarakani,kwa kipindi kifupi tumepata Vituo vitano vya afya ambapo awali tulikuwa navyo viwili tu,miradi ya maji ipo iliyokamilika wananchi wanapata huduma na mingine inaendelea ikiwa katika hatua mbalimbali za utekelezaji," amesema Mhe.Katani
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa