Na Kitengo cha Mawasiliano
Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Mwl.Sosthenes Luhende amewasistiza wanafunzi washiriki wa mashindano ya Umoja wa Michezo Shule za Sekondari Tanzania (Umisseta) kuwa na juhudi pamoja na kuzingatia nidhamu kipindi chote cha mashindano
Amesema hayo wakati akizindua mashindano ya Umisseta ngazi ya Wilaya Mei 27,2023 katika Shule ya Sekondari ya Tandahimba ambapo pia amekabidhi vifaa mbalimbali vya michezo ambavyo vimetolewa na Shirika la Sport Development Aid (SDA)
Naye Mratibu wa Umiseta Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Mwl.Laurian Chuwa amesema kuwa wamejipanga mapema kuhakikisha Hlmashauri inakuwa na uwakilishi mzuri katika mashindano kuanzia ngazi ya Mkoa,Taifa na Afrika Mashariki
Aidha amesema kuwa mashindano hayo yameshindanisha michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu,mpira wa pete,mpira wa mikono,mpira wa wavu,riadha na kuruka ambapo kati ya wanafunzi walioshiriki mashindano ya Wilaya 273 waliochaguliwa ni wanafunzi 100 ambao watakaa kambi kujiandaa na mashindano ya Umisseta ngazi ya Mkoa yanayotarajiwa kufanyika Juni 1 hadi 6,2023 katika uwanja wa Chuo cha Ufundi Mtwara
Mashindano haya Kitaifa yanatarajiwa kufanyika Mkoani Tabora na mashindano haya kwa Afrika Mashariki yatafanyika nchini Rwanda ambapo kauli mbiu ya mwaka 2023 "Uimarishaji wa Miundombinu ya Elimu Nchini Chachu ya Maendeleo ya Taaluma,Sanaa na michezo"
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa