Na Kitengo cha Mawasiliano.
Madiwani na baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe wakiwa wameongozana na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mhe.Fatma Nyangasa wamefanya ziara ya kujifunza Uzalishaji wa kilimo bora cha Korosho Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba.
Baada ya kuwasili katika Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Disemba 14,2023 Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala aliwasomea taarifa fupi ya Wilaya kisha wataalamu waliwasilisha mada muhimu za uzalishaji wa Korosho.
Wakiwa Tandahimba wametembelea kitalu cha miche ya korosho Kata ya Tandahimba,Shamba la Mikorosho Kitama,kujifunza mfumo wa stakabadhi ghalani Chama cha msingi Namunda na Kiwanda cha Ubanguaji Korosho TDC.
Aidha akizungumza kwa niaba ya Timu ya Wilaya ya Kisarawe Dc Nyangasa amepongeza juhudi zinazofanywa na Serikali katika zao la Korosho ambapo pia aliwapongeza wataalam wa Halmashauri ya Tandahimba wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti kwa kufanikisha ziara yao.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Mhe. Rehema Liute amewapongeza kwa kuchagua Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba kuja kujifunza ambapo amesema kuwa ziara yao ikalete matokeo chanya kwenye Halmashauri yao.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa