Na Kitengo cha Mawasiliano.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Mhe Baisa Baisa na Waheshimiwa Madiwani wa Kata zote 32 za Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba pamoja na wataalamu mbalimbali kutoka Halmashauri wamefanya ziara kata kwa kata wakihamasisha wazazi kuwapeleka watoto Shuleni pamoja na Kuhamasisha Wananchi kulima Mazao Mbadala ili waweze kujikwamua kiuchumi kuliko kutegemea zao Moja la Korosho.
Katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Tandahimba Diwani wa Kata ya Litehu Mhe. Seif Ahmad Nakuchima amewasisitiza wazazi kuhakikisha watoto waliofikia Umri wa kwenda Shule wapelekwe Shuleni wapate haki yao ya kupata Elimu.
Aidha, Afisa Elimu Kata ya Tandahimba Mohamed Mtesa amesema ni haki ya kila Mtoto kupata Elimu na Serikali ya Awamu ya Sita imeshajenga Miundombinu tayari kwa ajili ya Wanafunzi.
Kwa Upande wake Afisa Kilimo Haroun Kisimba amewasisitiza Wananchi kulima Mazao Mbadala na kuacha kutegemea zao la Korosho peke yake na badala yake walime Mbaazi na Ufuta kwa kuwa ni mazao yenye soko la uhakika na tayari yanauzwa kwa Mfumo wa Stakabdhi ghalani.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa