Na Kitengo cha Mawasiliano
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Mhe.Baisa Baisa amewasistiza .madiwani kusimamia miradi ya maendeleo inayotekelezwa ilkwenye maeneo yao ili iweze kukamilika na kutumika kwa wakati.
Amesema hayo.mara baada ya madiwani kuwasilisha Taarifa za maendeleo ya Kata zao leo Januari 11,2024 kwenye Mkutano wa Baraza la madiwani robo ya pili 2024/25 uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri.
" Miradi inapokuja kwenye Kata yako jukumu la Diwani ni kuhakikisha anausimamia mradi huo ukamilike ili wananchi wa eneo lako wafaidike nao," amesema Mwenyekiti Mhe.Baisa.
Aidha katika mkutano huo madiwani wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kusimamia bei ya korosho ambayo imeuzwa kwa bei ya juu lakini pia wamekiomba Chama kikuu cha Ushirika TANECU kushirikiana na ofisi ya Ushirika kushughulikia changamoto ya.malipo kwa baadhi ya wakulima.
Kwa upande wake mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya Ndg.Francis Mkuti akitoa salamu za Mkuu wa Wilaya kwa madiwani amesema madiwani wahimize wazazi na walezi kuwapeleka watoto shule zinapofunguliwa Januari 13,2025 kuanza masomo na kuhakikisha chakula kinapatikana shuleni, kutumia mvua zinazonyesha kulima mazao ya chakula,ukusanyaji wa mapato,utunzaji wa mazingira pamoja na kuendelea kuimarisha ulinzi na Usalama kwenye.maeneo yao.
Naye mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara Edith Shayo amewapongeza madiwani kwa kumaliza uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa amani na usalama ambapo ametoa wito kwa madiwani kuwasistiza wananchi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa