Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Michael Mntenjele ametembelea Kituo Cha Afya Mihambwe kwa ajili ya kuona hatua za ukamilishaji wa Ujenzi wa kituo hicho ambacho kinatarajiwa kutoa huduma kuanzia Septemba 23, 2024.
"Hakikisheni mnakamilisha vitu vilivyobaki kwa wakati ili Wananchi wapate huduma, majengo yatakuwa na maana kama yatatoa huduma za Afya kwa Wananchi" amesisitiza
Kwa Upande wake Diwani wa Kata ya Mihambwe Mhe.Abdurahim Mnyoroka ameishukuru Serikali kwa kusogeza huduma za Afya karibu na Wananchi wake.
Katika hatua nyingine DC Mntenjele ametembelea mradi wa Maji Chitoholi ili kuona Maendeleo ya hupatikanaji wa maji kwa Wananchi tangu ulipokamilika.
Mradi huo umegharimu Tsh.Bilioni 1.48 ikiwa ni fedha kutoka Serikali kuu kupitia mradi wa P-for-R ambapo zaidi Wananchi Elfu 10 kwenye vijiji Sita wananufaika na huduma ya Maji.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa