Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Tandahimba Ally Machela ameitaka Kamati ya usimamizi ya Hospitali ya Wilaya kutekeleza majukumu yao ili kuendelea kuboresha huduma kwa jamii
Ameyasema hayo jana wakati akizindua Kamati ya Usimamizi wa Hospitali ya Wilaya ya Tandahimba ambayo itafanya kazi kwa kipindi cha miaka mitatu
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Ally Machela akizindua Kamati ya Usimamizi ya Hospital
“Tunategemea kamati hii mtatekeleza majukumu yenu ikiwa pamoja na kuhakikisha wakazi wanapata huduma za afya zinazostahili na wanazozimudu kwa kufuata muongozo ,taratibu na kanuni,”amesema Machela
Katibu wa Hoapital Faustine Pamba(aliyesimama) akisoma majukumu ya kamati hiyo kwa Wajumbe
Naye Mganga Mkuu wa Hospital ya Wilaya Antipas Swai amesema kuwa Kamati hiyo ni moja ya kamati muhimu ndani ya hospital ya Wilaya hivyo inajukumu ya kuimarisha uhusiano na wadau mbalimbali katika kuboresha usimamzi wa huduma
Mganga Mkuu wa Hospital ya Tandahimba Antipas Swai (aliyesimama)akitoa neno
Aidha baada ya uzinduzi huo wajumbe walimchagua Mwenyekiti ambaye ataongoza Kamati hiyo kwa kuda wa miaka mitatu ambapo Adinani Mbwana alifanikiwa kuchukua kiti hicho
Mwenyekiti wa kamati ya usimamizi ya Hospitali Adinani Mbwana akitoa neno kwa Wajumbe
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa