Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Tandahimba imefanya ziara ya siku mbili ya kutembelea miradi ya maendeleo inayotekelezwa ndani ya Wilaya na kuridhishwa nayo
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Tandahimba Omari Nang'uta (kulia) akikagua mradi wa zahanati ya Miuta
Katika ziara ya kamati ya siasa ambayo iliongozwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Tandahimba ndg. Omari Nang’uta ,aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala,Mbunge wa Jimbo la Tandahimba Mhe.Katani Katani, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ndg. Said Msomoka na wakuu wa idara na vitengo walitembelea miradi ambayo inaendelea kutekelezwa katika kat a mbalimbali ndani ya Wilaya
Kamati ya siasa,Dc Sawala ,Mkurugenzi na wakuu wa idara wakifurahia jambo
Akitoa majumuisho ya ziara hiyo ya siku mbili Mwenyekiti wa CCM Wilaya amesema kamati imeridhishwa na miradi hiyo lakini kuna baadhi ya miradi inahitaji usimamizi wa ziada ili imalizike kwa wakati iwanufaishe wananchi wa eneo husika kwa wakati
Kamati ya siasa ,Mbunge,na wakuu wa Idara wakikagua miradi
“Tumeiona miradi inakwenda vizuri lakini ipo baadhi inasuasua sisi tuombe usimamizi uendelee ili miradi imalizike kwa wakati wananchi waweze kupata huduma hiyo ,”amesema Mwenyekiti
Mradi wa Maabara Mdimba sekondari ambao upokwenye hatua za mwisho
Naye Dc Sawala amesema kuwa katika kutekeleza miradi ushirikiano na mawasiliano kwa wahusika wanaosimamia miradi inakuwa ni chachu ya miradi kumalizika kwa wakati na kuwa bora
Dc Sawala akieleza jambo
Aidha naye Mhe.Katani Katani amesema pamoja na miradi hii kuwa bora na baadhi kusua sua jukumu la wasimamizi wa miradi ni kuhakikisha wazabuni wanaleta vifaa kwa wakati eneo la mradi ili wananchi washiriki kikamilifu katika miradi yao
Mbunge wa Jimbo la Tandahimba Mhe.Katani akielezea jambo kwenye ujenzi wa mradi wa sekondari ya Mndumbwe
Mkurugenzi Mtendaji ndg Msomoka amewahikikishia kamati ya siasa kuwa pale ambapo yameonekana mapungufu yatarekebishwa , usimamizi na ufuatiliaji utakuwa wa mara kwa mara ili miradi iwe bora na imalizike kwa wakati kwakushirikiana na wataalam
Mkurugenzi Mtendaji ndg Said Msomoka akiwa na wataalam na kamati kwenye mradi wa sekondari ya Litehu
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa