Na Kitengo cha Mawasiliano.
Kamati ya Lishe Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba leo Novemba 6,2023 imejadili utekelezaji wa afua za lishe kwa kipindi cha robo ya kwanza kuanzia Julai hadi Septemba,2023
Akizungumza kwenye kikao hicho kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Ndg.Raphael Mputa amesema ili jamii iweze kufanya shughuli za kimaendeleo inahitaji kuwa na afya bora hivyo amesistiza elimu iendelee kutolewa kwa jamii kuhusu afya na lishe.
" Elimu iendelee kutolewa kwa jamii kuhusu afya na lishe sambamba na kuyatekeleza yale ambayo tumekubaliana katika kikao hiki ," amesema Mputa
Aidha katika kikao hicho Divisheni na vitengo ziliwasilisha taarifa za utekelezaji wa afua za lishe kwa kwa kipindi cha robo ya kwanza ambapo Kamati zilijadili taarifa hizo .
Naye Mganga Mkuu Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Dr.Grace Paul amesema timu za wataalamu wa afya na lishe wameendelea kutoa elimu kwa jamii katika Kata na Vijiji
Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba kupitia kamati ya lishe na viongozi mbalimbali wamekuwa Mstari wa mbele katika kuhamasisha na kutoa Elimu ya lishe ili keuepuka Udumavu na kujenga Jamii yenye Afya Bora.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa