Na Kitengo cha Mawasiliano
Kamati ya Fedha ,Utawala na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba imeridhishwa na Kasi ya Ujenzi wa Vyumba kumi vya madarasa unaoendelea ikiwa ni maandalizi ya Kidato cha Kwanza mwaka 2023
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Mhe.Baisa Baisa Novemba 3,2022 baada ya kutembelea na kukagua miradi ya Maendeleo kwa kipindi cha Robo ya kwanza mwaka 2022/2023
“Tumetembelea miradi nane ya Maendeleo ya Afya na Elimu ,lakini katika Elimu tumetembelea ujenzi wa v yumba kumi vya madarasa ambapo fedha tumepokea mwezi wa kumi kwa ajili ya maandalizi ya kidato cha kwanza mwakani,ujenzi wa madarasa hayo unakwenda kwa kasi na ubora sisi kamati tumeridhishwa kwa hilo na tunamshukuru Mhe.Rais kwa fedha za ujenzi wa madarasa,”amesema Mwenyekiti
Miradi iliyotembelewa na Kamti ya Fedha ni Ukarabati wa Wodi ya Kutengwa iliyopo Hospitali ya Wilaya ya Tandahimba,Ujenzi wa Kituo cha Afya Mihambwe,Ujenzi wa Zahanati ya Chikongo,Ujenzi wa Vyumba vitatu vya madarasa shule ya Sekondari Kwanyama
Aidha Miradi mingine iliyotembelewa ni Umaliziaji wa Ujenzi wa Zahanati ya Dinduma,Ujenzi wa vyumba vitatu vya Mdarasa Shule ya Sekondari Mndumbwe,Ujenzi wa vyumba vine vya madarasa Shule ya Sekondari Tandahimba na Ujenzi wa Marasa mawili ya Awali ya Mfano Shule ya Msingi Mjimpya iliyopo Kata ya Tandahimba
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa