Pichani: Kamati ya Siasa Mkoa wa Mtwara ikiwa kwenye picha ya pamoja na Kamati ya CCM Wilaya ya Tandahimba
Na Afisa Habari
Kamati ya Siasa Mkoa wa Mtwara imefanya ziara kukagua miradi ya maendeleo leo wilayani Tandahimba na kuridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo“Tumeiona,tumeridhishwa,kazi nzuri,inatia moyo”,Alhaj Saidi Kusilawe, Katibu wa CCM Mkoa wa Mtwara alisema.
Akizungumza wakati wa majumuisho baada ya ziara hiyo, Katibu huyo alisema kuwa Chama cha mapinduzi kimeamua kufanya ziara na kukagua miradi ya maendeleo kikiwa kinaelekea kilele cha maadhimisho kumbukizi ya miaka 43 tangu kuanzishwa ambapo kimkoa siku hiyo itaadhimishwa wilaya ya Mtwara vijijini katika Tarafa ya Nanyamba, Jimbo la Nanyamba tarehe 08.02.2020, “Ni Imani yangu nyote tutajumuika na karbuni tukienzi Chama cha Mapinduzi”, Kusilawe alisema.
Alhaj Kusilawe amewapongeza watendaji wilaya ya Tandahimba kwa kusimamia na kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi hususan ujenzi wa miradi ya maendeleo licha ya changamoto zinazoikabili wilaya hiyo; ametoa rai kwa watendaji kushirikiana na kushikamana kati ya chama na serikali ili kuwaletea wananchi maendeleo.
Kamati ya Siasa CCM mkoa ilibaini changamoto ya utekelezaji wa miradi ya barabara inayosimamiwa na TARURA ya mfumo unaotumika kuwapata Wakandarasi ambapo huratibiwa na kusimamiwa na ngazi ya mkoa na kuwataka Mameneja wa wilaya kusimamia ujenzi wa miradi hiyo hali inayopelekea kukosa nguvu ya kuwawajibisha pindi wakandarasi wanapokiuka mkataba wa makubaliano.
Katika ziara hiyo Kamati ya siasa mkoa wa Mtwara ilifanikiwa kukagua ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa shule ya msingi Lidumbe Mtoni na ukamilishaji wa vyumba viwili vya madarasa katika shule ya msingi Nanhyanga.
Aidha Kamati hiyo ilikagua mradi wa umeme wa REA kijiji cha Nakayaka kata ya Chikongola pamoja na ujenzi wa Kalvati barabara ya Tandahimba – Mivanga na kumalizia jengo la Wadhibiti Ubora wa elimu wilaya.
Kamati ya siasa mkoa wa mtwara ikitoa maelekezo kwa Watendaji baada ya kukagua ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa shule ya msingi Lidumbe Mtoni
Kamati ya siasa mkoa wa mtwara ikijionea mradi wa Umeme wa REA kijiji cha Nakayaka kata ya Chikongola
Huo ni mradi wa ukamilishaji wa vyumba viwili vya madarasa shule ya msingi Nanhyangaambapo Kamati ya siasa mkoa wa mtwara ilipata fursa kujionea
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa