Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Sostenes Luhende ameongoza Kikao Cha Kamati ya lishe Robo ya Tatu ambapo amewasisitiza Viongozi wa vijiji kutoa Elimu kwa jamii kuzingatia mlo kamili ili kuepuka udumavu na sio kujaza tumbo.
Aidha, Luhende amesisitiza pia Walimu kuhakikisha Chakula kinatolewa Shuleni ili Wanafunzi wapate Chakula na kuendelea na Masomo.
Kwa Upande wake Afisa Lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Asha Selemani amesema kupitia Idara na vitengo mbalimbali ikiwemo Elimu, kilimo na Ufugaji zimeweza kutekeleza shughuli za lishe kwa ufanisi.
Baadhi ya wajumbe wa Kikao hicho wameshauri Bajeti iliyotengwa Kwa ajili ya utekelezaji wa afua za lishe ikiwemo mashamba Darasa ya Ufugaji na kilimo hasa Shuleni iweze kutumika ili kuleta ufanisi na uboreshaji Afya kwa jamii.
#kaziiendelee
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa