Na Kitengo cha Mawasiliano
Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba imeadhimisha kilele cha siku ya Vijana kwa kutoa Elimu kwa vijana kutumia fursa zilizopo ndani ya Halmashauri ili kukuza uchumi wao
Wakipewa Elimu hiyo katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ,vijana wamepewa elimu kuhusu mikopo ya asilimia 10 inayotolewa katika Halmashauri ambapo wakitumia fursa hiyo itawasaidia kukuza uchumi wao kwa kuwa mikopo hiyo haina riba
Katika maadhimisho hayo Vijana wamepewa Elimu ya kusajili vikundi na elimu ya afya ili kujenga vijana wenye afya bora sambamba na kusikiliza changamoto zao
Aidha katika maadhimisho hayo yenye kauli mbiu 'Kila Mmoja Anahusika Kujenga Uchumi Imara ,Ustawi na Maendeleo Endelevu,Jiandae Kuhesabiwa' vijana waliamasishwa umuhimu wa kushiriki katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi Agosti 23,2022 ili kupata takwimu sahihi kwa ajili ya Mipango ya Maendeleo
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa