Na Kitengo cha Habari na Mawasilinao
Halmashauri ya Tandahimba imetoa shilingi Milioni 40 kwa ajili ya ukarabati wa vyumba viwili vya madarasa kwa shule ya Msingi Mkonjowano ambavyo vimeezuliwa na upepo iliyoambatana na mvua na kusababisha wanafunzi 143 kukosa madarasa ya kusomea
Mkuu wa Wilaya akionyesha jinsi ofisi ya walimu ilivyoharibika baada ya maafa hayo
Akizungumza kwenye eneo la tukio Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba alimtaka Mkurugenzi kuharakisha ukarabati wa majengo hayoa na kusistiza kuendelea kupanda miti kwenye maeneo ya shule kwasababu mvua huambatana na upepo mkali hivyo miti inasaidia kupunguza makali
Chumba cha darasa la tatu , darasa la nne na ofisi ya walimu inavyoonekana baada ya kuezuliwa na upepo
‘Uhalibifu huu ni mkubwa lakini miti hii iliyopo imesaidia kupunguza makali ya upepo kungekuwa hakuna miti kama hii athari ingekuwa kubwa zaidi kwaiyo endeleeni kuchukua tahadhari na mzingatie kupanda miti mvua hizi zinapokuja zinaambatana na upepo mkali sana kama maeneo hayana miti maafa yanakuwa makubwa zaidi,”amesema Dc Waryuba
Dc Waryuba (kulia)akizungumza na viongozi wa kata hiyo
Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji ndugu Ally Machela baada ya kutembelea eneo hilo akiwa ameambatana na Afisa Elimu Msingi na Mwenyekiti wa Halmashauri walishuhudia uharibifu ulifanyika katika shule hiyo
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Ally Machela
“Tumetembelea tukaona hali ilivyo Halmashauri imetoa kiasi cha shilingi milioni 40 kwa ajili ya vyumba hivyo vya madarsa viweze kukarabatiwa kwa haraka ili wanafunzi waendelee na masomo kwenye madarasa yao,tayari mafundi wameanza kazi,”amesema Ndg Machella
Mwenyekiti wa Halmashauri Baisa Baisa (wapili kushoto) akiwa na Kaimu Mkurugenzi Ally Machela(watatu kushoto) ,Afisa Elimu na waheshimiwa madiwani ambao walitembelea eneo hilo
Naye Afisa Elimu Msingi Bi Hadija Mwinuka amesema kuwa kwa sasa wananfunzi hao wa darasa la tatu na nne ambao madarasa yao yameezuliwa wanaendelea na masomo kwenye madarasa mengine huku utaratibu wa kuharakisha ujekarabati wa madarasa yao unaendelea
“Madarasa ambayo yameezuliwa ni darasa la tatu na la nne lakini wanaendelea na masomo tulichofanya ni wanafunzi wa darasa la kwanza na la pili wanaingia kwa kubadilishana wengine asb na wengine mchana
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa