Na Kitengo Cha Habari na Mawasiliano
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Tandahimba Said Msomoka ametoa eneo kwa ajili ya Mtandao wa kijani Kibichi Tanzania (Mkikita) kujenga kiwanda na ghala la kisasa kwa ajili ya wakulima wa korosho
Akizungumza ofisini kwake Msomoka amesema kuwa kiwanda kitakachojengwa kitawasaidia wakulima kuweza kuuza korosho zao ambazo zimebanguliwa na ambazo bado kwa kuwasogezea huduma
“Tunawakaribisha katika Wilaya yetu na tunawapa eneo kwa ajili ya kiwanda na ghala kwasababu tunajua kitakuwa msaada mkubwa kwa wakulima wetu,hata hivyo tunawakaribisha wawekezaji waje kuwekeza Tandahimba maeneo yapo kwa ajili ya uwekezaji,”amesema Msomoka
Aidha amesema kuwa mbali na ujenzi huo Mkikita wanatarajia kuboresha thamani ya korosho kwa kutoa pembejeo na mbinu mbalimbali kwa wakulima ambapo wanatarajia kuingia mkataba na Umoja wa wakulima korosho Tandahimba(Uwokota) na Kitama Farmers
Naye Mkurugenzi wa Mtandao wa Kijani Kibichi (Mkikita) Adam Ngamange amesema kuwa lengo ni kuongeza thamani ya zao la korosho sambamaba na kuwashawishi wawekezaji wa viwanda na kufungua kliniki ya kilimo ya mazao mbalimbali
“Lengo la mtandao wetu wa kijani kibichi ni pamoja na kuongeza thamani ya korosho ,kujenga kliniki ya kilimo kwa mazao mbalimbali ,kutoa mafunzo yanayohusu kilimo sambamba na kuwapa mitaji,pembejeo ,ushauri kuhusu mazao na kutafuta masoko,”amesema Ngamange
Hata hivyo naye Mwenyekiti wa Umoja wa wakulima korosho Tandahimba(Uwokota) Shabia Kajete amesema uwekezaji huo utawasaidia wakulima kupata huduma bora karibu yao
“Mtandao huu ukijenga kiwanda na ghala utatusaidia sisi wakulima kwakuwa wakulima wengine wanabangua korosho zao lakini wanakosa mahali pa kupeleka korosho hizo lakini sasa hivi watapunguza tatizo hilo kwa wakulima,”amesema Kajete
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa