Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mtwara imeipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba kwa ujenzi wa ofisi 41 za walimu
Shule shikizi Amani iliyopo kata ya chaume
Mbunge wa Jimbo la Tandahimba Mhe.Katani Katani akieleza kwa kamati ya siasa jinsi shule shikizi zinavyowasaidia watoto wanatembea umbali mrefu
Pongezi hizo zimetolewa na Kamati ya siasa Januari 21,2022 ilipotembelea utekelezaji wa miradi ya maendeleo ndani ya Halmashauri ya Tandahimba,Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mtwara ndugu Yusuf Nannila amesema jukumu liliopo ni wanafunzi kuhakikisha wanaongeza bidii kwenye masomo ili kuongeza ufaulu katika Wilaya na Mkoa kwa ujumla
Kamati ya siasa ikitembelea miradi mbalimbali ya maendeleo
“Tumefanya ziara ya kutembelea miradi inayotekelezwa na ilani ya ccm,tunaipongeza Halmashauri ya Tandahimba kwa kumaliza miradi ya vyumba vya madarasa kwa wakati na kujiongeza kwa kujenga ofisi 41 za walimu ambazo zitawasaidia walimu kukaa katika mazingira bora,nawapongeza sana kwa hatua hii,”amesema Mwenyekiti
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mtwara ndugu Yusuf Nannila akieleza jambo kwa wananchi wa Mambamba (hawapo pichani) kwenye kituo cha afya cha Mambamba
Aidha katika ziara hiyo kamati ya siasa ilitembelea miradi ya elimu,afya na barabara ambapo imeridhishwa na utekelezwaji wake na kusistiza kuwa pale ambapo yameonekana mapungufu madogo madogo yarekebishwe kwa wakati sambamba na hilo imeagiza wakandarasi wa ujenzi wa barabara ya Natosa kuhakikisha ujenzi unakamilika kwa wakati
Kamati ya siasa wakikagua ujenzi wa barabara ya Natosa inayojengwa kwa lami ikiwa inaendelea na ujenzi huo
Naye Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe.Brigadia Jenerali Marco Gaguti ambaye alikuwa kwenye ziara hiyo amehimiza wananchi kuhakikisha wanafunzi wote wanakwenda shule na kuongeza bidii kwenye masomo yao
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe.Brig.Jen.Marco Gaguti akiwahimiza wananchi wa kata ya Chaume Halmashauri ya Tandahimba kuhusu elimu
“Mkoa wa Mtwara suala la elimu bado lipo chini,niwaombe wazazi na walezi kuhakikisha wanafunzi wanahudhuria shule ambazo tayari zimefunguliwa kuanzia Januari 17,2022 lakini pia waongeze bidii katika masomo ili waweze kufikia malengo yao,”amesema Rc
Wakuu wa Idara na Vitengo wakiwa kwenye majumuisho ya ziara ya kamati ya siasa Mkoa wa Mtwara katika ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba
Aidha wanafunzi wa Wilaya ya Tandahimba wameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa ujenzi wa vyumba vya madarasa 88 na kuahidi kuongeza bidii kwenye masomo yao ili waweze kufikia malengo yao
Wanafunzi wa sekondari ya Nandonde wakiwa darasani miongoni mwa madarasa saba yaliyojengwa katika shule hiyo
Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba ilipata kiasi cha shilingi Bil.1.76 fedha za mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya uviko-19 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 88 vya madarasa ambapo ilijiongeza kwa kujenga ofisi za walimu 41 ambazo zimekwenda sambamba na ujenzi wa vyumba hivyo vya madarasa
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Tandahimba ndugu Mussa Gama akifafanua jambo kwa wajumbe wa kamati ya siasa Mkoa
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa