Na Kitengo cha Mawasiliano
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Ndg.Mussa Gama amewasistiza Watendaji Kata kuhakikisha wanafunzi walioandikishwa wanahudhuria shule lakini pia wanafunzi wa madarasa mengine
Amesema hayo Januari 12,2023 wakati akizungumza na Watendaji Kata zote 32 zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba katika kikao kazi kilichofanyika ukumbi wa mikutano wa Halmasahauri
Watendaji Kata wakiwa katika kikao kazi
“Hali ya Uandikishaji kwa darasa la kwanza hadi sasa ni asilimia 96 na awali ni asilimia 88 lengo tufikie asilimia 100 nawasistiza katika maeneo yenu hakikisheni wote walioandikishwa wanahudhuria shule,lakini hata madarasa mengine ya shule za Msingi na Sekondari na hatua zichukuliwe kwa wanafunzi watoro,”amesema Mkurugenzi
Aidha amewasistiza kuongeza kasi katika usimamizi wa miradi ya Maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao,Utekelezaji wa afua za lishe,usafi wa mazingira,ukusanyaji wa mapato,usafi wa mazingira na kila kata ipande miti isiyopungua thelathini (30) katika shule,zahanati,vituo vya afya,ofisi za kata na vijiji katika kipindi hiki cha msimu wa mvua
“Nawapongeza kwa kipindi cha nusu mwaka mmeweza kusiammia na kutekeleza yale ambayo tuliazimia sasa twende na kasi zaidi tukayatekeleze katika vipindi hivi viwili vya kumaliza mwaka wa fedha,”Mkurugenzi
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Utumishi na Rasilimaliwatu Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Bi.Jane Mallongo ametoa wito kwa Watendaji Kata kuendelea kuzingatia Miongozo,taratibu,sheria na kanuni za Utumishi wa Umma katika kutekeleza majukumu yao
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa