Na.Kitengo cha Mawasiliano
Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Dkt.Grace Paul amehudhuria Maadhimisho ya Siku ya Afya na Lishe ya Kijiji Cha Mkola chini Kata ya Luagala na kuwapongeza wananchi kwa juhudi na mwamko wa kuzingatia Lishe kwa watoto na wajawazito huku akivitaka Vijiji vingine kuiga Mfano huo ili kuweza kujenga Jamii Bora na yenye Afya.
Amesema hayo Septemba 26,2023 kwenye maadhimisho ya Siku ya Afya na Lishe yaliyofanyika katika katika kijiji hicho ambapo amewasisitiza wananchi wa kijiji hicho kuhakikisha familia zao zinakula Chakula Bora kwa kuzingatia makundi matano ya Chakula.
Kwa Upande wake Diwani Viti maalumu Kata ya Luagala Mhe.Mariam Damla amewaasa wananchi kuadhimisha siku ya lishe kwa vitendo kila siku na si kusubiri Maadhimisho.
Aidha, Afisa Lishe Wilaya ya Tandahimba Ndg Asha Selemani ametoa Elimu ya matumizi ya chumvi yeye madini joto,makundi matano ya chakula na mapishi ya uji ulioboresha kwa ajili ya watoto na wajawazito huku akitoa wito kwa wananchi wa Vijiji vyote vya Tandahimba kuwapa watoto Mlo kamili ili kuepuka Udumavu kwa watoto hao.
Maadhimisho ya Siku ya Afya na lishe ya Kijiji yenye Kauli mbiu isemayo "LISHE BORA NI MSINGI WA MAENDELEO" yanaendelea kuadhimishwa katika Vijiji vyote vya Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba katika kipindi cha robo ya kwanza ya Mwaka 2023/2024 .
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa