Na Kitengo cha Mawasiliano
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Ndg. Mariam Mwanzalima amewataka wanafunzi wa kozi ya awali ya Jeshi la Akiba kuzingatia nidhamu na kujifunza kwa bidii kwa kipindi chote cha mafunzo
Amesema hayo Agosti 25,2024 wakati akifungua mafunzo ya kozi ya awali ya Jeshi la akiba kwenye Kata ya Mkundi iliyopo Tarafa ya Mahuta
" Katika kipindi chote ambacho mtakuwa katika mafunzo haya zingatieni nidhamu na mjifunze kwa bidii ili mkihitimu kozi hii mkailinde Nchi,watu na Mali zao," amesema Mkurugenzi Mwanzalima
Kwa upande wake Mshauri wa Jeshi la Akiba Wilaya ya Tandahimba Meja Kalist Simon amesema kuwa kozi hiyo ya awali ya Jeshi la akiba itakuchua muda wa wiki 18 ambapo ina jumla ya wanafunzi 72
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa