Na Kitengo cha Mawasiliano.
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala amewahimiza wanafunzi kusoma kwa bidii ili kufikia malengo yao na kuleta Maendeleo katika Wilaya na Taifa kwa Ujumla.
Akizungumza na Wanafunzi hao kwa nyakati tofauti mwishoni mwa wiki Dc Sawala amesema Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kuboresha mazingira bora ya ufundishaji na ujifunzaji kwa Shule za Sekondari na Msingi ni wajibu wa wanafunzi kusoma kwa bidii.
"Serikali imeendelea kuboresha mazingira bora ya ufundishaji na ujifunzaji ni wajibu wenu wanafunzi kusoma kwa bidii ili mfikie malengo mliyojiwekea,hakuna njia mbadala ya kufikia malengo yako bila kusoma kwa bidii," amesema Dc Sawala
Aidha amewasistiza wazazi na walezi kuhakikisha wanafunzi wanakwenda shule ili kuepuka utoro wa reja reja na wakudumu kwa wanafunzi huku akiwataka wazazi na walezi kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula shuleni.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa