Na Kitengo cha Mawasiliano
Kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Machi 8,2023 Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mkhe.Kanali Patrick Sawala ametoa wito kwa wanawake kuwa karibu na watoto ili kubaini changamoto zao sambamba na kupinga ukatili na unyanyasaji wa kijinsia kwa jamii
Ameyasema hayo Februari 24,2023 wakati akizungumza na wanawake wa Tandahimba waliojitokeza kwa wingi katika viwanja vya nje ya ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ambapo amesema kuwawanawake wananyanyasika lakini baadhi hawataki kutoa taarifa
“Wakina mama kuweni karibu na watoto ili kujua changamoto zao,ni wakati wa kusema unyanyasaji wa kijinsia na ukataili sasa basi,Serikali ipo na nyinyi,kuna madawati ya kijinsia ,msikae kimya mnapoteza haki zenu toeni taarifa katika vyombo husika ili hatua zichukuliwe,”amesema Dc Sawala
Aidha Dc Swala alisikiliza kero mbalimbali zilizotolewa na wanawake ambapo alizitolea ufafanuzi na zingine aliahidi kuzifuatilia kwa hatua Zaidi,alitumia nafasi hiyo kuwapongeza wanawake kwa jinsi wanavyoshiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo pia amewasistiza kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mapokezi ya Mwenge wa Uhuru Aprili5,2023 na kushiriki kilele cha siku ya wanawake Machi 8 ambayo yatafanyika Kimkoa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba
Naye Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Ndg.Mussa Gama akizungumzia uwezeshaji wanawake kiuchumi amesema Halmashauri inatoa asilimia nne (4) kwa wanawake ambapo amewasistiza kulipa mikopo hiyo kwa wakati ili wanawake wengine wanufaike nayo
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa