Na Kitengo cha Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala ametoa wito kwa walimu wa mazoezi kutoka Chuo cha Ualimu Mtwara Ufundi ambao wamepangiwa kwenye shule zenye upungufu wa walimu katika Halmashauri ya Tandahimba kuendelea kuzingatia maadili ya ualimu
Akizungumza na walimu hao 151 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri Januari 21,2023 Dc Sawala amesema kuwa kwa kipindi cha miezi miwili ambacho watakuwa katika shule hizo tunatarajia kuona mabadiliko kwa wanafunzi
“Nendeni mkafanye kazi kwa kuzingatia maadili ya ualimu ,Mimi nawahakikishia kwanza Usalama wenu,Ulinzi wenu,hakuna atakayechezea kada yenu na hakuna atakayekuzuia kufanya kazi yako kwa maslahi yake binasi,nendeni mkafanye kazi mkiwa mnajiamini mpo sehemu salama,Karibuni Tandahimba,”amesema Dc
Aidha amewasistiza kuwa wastahimilivu na kubainisha kuwa sifa mojawapo ya mwalimu ni kiongozi hivyo watakutana na wanafunzi tofauti tofauti jukumu la mwalimu ni kuwafundisha maadili nao waweze kuwa bora zaidi
Naye Mkuu wa Idara ya Elimu ya Awali na Msingi Ndg.Samweli Mshana akisoma taarifa yake fupi amesema kuwa kwa kipindi ambacho watakuwepo katika shule hizo mahitaji ya msingi yameandaliwa kwa ajili yao
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa